IDARA YA VIJANA

MAONO:  Kuwa na vijana wenye nguvu za kiroho na kiuchumi wanaoishi katika Hatma zao ndani ya pendo la Kristo.

MALENGO:

–         Kila kijana kukua katika vina vya maarifa ya Neno la Mungu na kuweka katika matendo.

–         Kila kijana kuwa thabiti kiuchumi ili aujenge Ufalme na yeye binafsi.

–         Kila kijana kujua na kuiishi Hatma yake,  huku akitumia vyema vipawa na vipaji alivyepewa na Mungu.

–         Kila kijana awafikie wengine kwa Injili ya Ufalme wa Mungu.

–         Kila kijana awe na ushirika mzuri na wenzake, kanisa na jamii kwa ujumla kupitia pendo la Kristo.

MIKAKATI:

  • Kuwawezesha vijana kushiriki vipindi vyao vya kila wiki, mikesha, kambi, uinjilisti, talk show, matamasha, talent show, makongamano ya vijana n.k kulingana na ratiba yao ya mwaka.
  • Kuwawezesha vijana kuwa na vikundi vidogo vidogo vya majadiliano ya biblia (bible groups) ili kukuza ufahamu wa kila mmoja katika Neno.
  • Kubuni miradi mbalimbali ya kimaendeleo kwa ajili ya kukuza uwezo wa kiuchumi wa kijana mmojammoja na kwa ujumla.
  • Kuwa na rekodi ya vijana wote (database) itakayotunza taarifa sahihi na kufanya mabadiliko (updates) kila inapobidi.
  • Kujitangaza na kuwafikia vijana wengine kwa kutumia mitandao ya kijamii kama facebook, instagram, tovuti, blogs k
  • Kuwa na vikundi vya wanataaluma, wafanyabiashara, wasanii ambao watafanya kazi pamoja ili kuleta matokeo makubwa.
  • Kuwa na Katiba rafiki itakayowezesha undeshwaji mzima wa idara ya vijana.

RATIBA YA VIJANA LWC MAKUTI KAWE (2016)

Ratiba ya Wiki:

Jumatano :    KIPINDI CHA VIJANA WOTE.

Kuanzia saa kumi na mbili na nusu jioni  hadi saaa mbili usiku

Ijumaa     :    MKESHA WA VIJANA WOTE

Ijumaa tatu za mwazo wa mwezi, kuanzia saa nne usiku hadi saa tisa usiku

Ratiba ya mwaka:

15 -16 Januari:         KAMBI YA VIJANA

28 Februari     :       UINJILISTI

09 Aprili        :         OPEN AIR CRUSADE

07 Mei            :       SAFARI YA MBUGA ZA WANYAMA

29 Mei            :       UINJILISTI

04 Juni            :       KUTEMBELEA HOSPITALI

10 -11 Juni     :        KAMBI YA VIJANA

11 Septemba  :        UINJILISTI

14 -15 Octoba:        KONGAMANO LA VIJANA

18 Disemba   :        SADAKA YA SHUKRANI YA VIJANA

18 Disemba    :       TATHMINI YA MWAKA