HUDUMA YA WANAWAKE WA LWC – KAWE

 

1.0         Utangulizi

Huduma ya Wanawake wa Living Water Centre – Kawe ilianzishwa rasmi mwaka 2001 na mtumishi wa Mungu, Mbeba maono Apostle Onesmo Ndegi ikiwa chini ya usimamizi wa Mama Lilian Ndegi.

2.0         Lengo la Huduma ya Wanawake LWC

Lengo kuu la huduma ya wanawake ni kuhakikisha kila mwanamke anakua na kuongezeka katika kiwango cha kumjua na kumpenda Mungu. Pia kuibua vipawa na karama ndani ya wanawake ili kila mmoja aweze kumtumikia Mungu kwa nafasi ambayo Mungu amemkusudia. Aidha, huduma hii ya wanawake wa LWC imekusudia kuwaleta wanawake pamoja katika kanisa kwa kusudi la kuujenga Ufalme wa MUNGU.

Ili kufanikisha lengo hili, mafundisho na programu mbalimbali huandaliwa kwa ajili ya wanawake katika kanisa ikiwa ni pamoja na: Makongamano ya wanawake ambayo hujumuisha:

 • Kongamano la Wanawake ambalo hujumuisha wanawake wote ndani na nje ya kanisa – Moyo wa  wanamke Conferences”
 • Semina za ndani ambazo hufanyika angalau mara moja kwa mwezi “Mwanamke wa Hekima Seminars” semina hizi hujumuisha wanawake wote wa makanisa ya LWC hasa waliopo Dar es Salaam
 • Kongamano kubwa la mabinti wote – hujumuisha mabinti wote wa ndani na nje ya kanisa, mara moja kwa mwaka –  “Binti na Ufahamu Bora” na
 • Vipindi vya wanawake kila wiki kukutana kujifunza mambo mbalimbali ya kiroho na kimwili ikiwa ni pamoja na:
  • Uchumi
  • Mahusiano
  • Malezi ya watoto na vijana
  • Ujasiriamali
  • Mapishi
  • Kazi za mikono n.k.

3.0         Huduma zilizopo ndani ya huduma ya Wanawake

Ndani ya huduma ya wanawake, zipo huduma na idara zinazofanya kazi chini yake ambazo ni kama ifuatavyo:

 • Huduma ya Mwanamke Mshunami;
 • Kazi kubwa ya huduma hii ni kuwategemeza watumishi wa Mungu
  • Huduma ya Uinjilisti;
 • Kazi kubwa ni kuweka mikakati ya kupeleka injili kupitia wanawake wote (huduma zote)
 • Kutunza kumbukumbu za watu wanaookoka katika ushuhudiaji/semina za ndani na makongamano ya kina mama.
  • Huduma ya Kugusa Jamii;
 • Huduma hii inalenga kuwasaidia watu wenye uhitaji waliomo ndani na nje ya Kanisa
 • Huduma ya Dorcas;
 • Huduma hii huwatambua yatima na wajane waliomo ndani ya kanisa na kuwawezesha kiuchumi na kufufua tumaini ndani yao.
  • Wanawake wa Ufalme wa Mungu (Wok);
 • Hii ni timu ya wanawake ya inayojihusisha na uimbaji – kusifu na kuabudu
  • Huduma ya Wabibi;
 • Huduma hii huwakusanya Wanawake Wazee ili katika uzee wao wajikite katika kumtumikia Mungu kwa maombi, uinjilisti na huduma mbalimbali katika Ufalme wa Mungu

4.0         Mafanikio Ya Huduma Ya Wanawake LWC

Baadhi ya Mafanikio ya huduma ya Wanawake wa LWC, ni kama ifuatavyo:

 1. Tumefikiana sisi kwa sisi kwa kusaidiana na kutiana moyo kwa  uhitaji wa kiroho na kimwili
 2. Tumewafikia Watoto, Vijana na Mabinti ndani na nje ya LWC .
 • Kupitia Semina na Makongamano, tumewafikia Wanawake wengi, wameokoka na wengi wamefunguliwa na kuwekwa huru mbali na vifungo mbalimbali kwa mfano:- Kongamano la Moyo wa mwanamke (ambalo hufanyika kila mwaka) limekuwa na mafanikio makubwa kila mwaka
 1. Ibada ya Mjini iliyoanzishwa na Wanawake wa LWC, imeendelea kukua na watu wengi kutoka madhehebu mbalimbali hufika kujifunza Neno na wengi wameokoka na kusimama – shukrani  za pekee kabisa kwa Baba na Mama Apostle Ndegi,  na wachungaji wote ambao wamekuwa na utayari mkubwa wa kuhudumu katika ibada  zetu za mjini –  Mungu awabariki sana)
 2. Kununua shamba la hekari 75 katika kijiji cha kurui, Wilaya ya Kisarawe
 3. Kupata eneo la hekari moja kwa ajili ya kujenga nyumba ya maombi katika eneo la Mabwe Pande
 4. Kuanzishwa kwa mfuko wa kuweka na kukopa “Mti Mbichi” ambapo wanawake wamejiwekea akiba na baadhi wameweza kukopa kwa shughuli mbalimbali za maendeleo

 

5.0         Mipango Na Mikakati Ya Baadaye

 1. Mwendelezo wa Semina za “Mwanamke wa Hekima” na Makongamano ya “Moyo wa Mwanamke” na “Binti na Ufahamu Bora”
 2. Kuimarisha huduma za Wanawake katika vituo vya Makanisa yote ya LWC Tanzania
 1. Huduma zilizo ndani ya Huduma ya Wanawake kuimarishwa na   kuboreshwa kwa kuhakikisha wanawake wengi zaidi wanahusika