Huduma ya Teenagers

UTANGULIZI

Living Water Centre ni huduma inayozangatia umuhimu  wa malezi na makuzi ya watoto katika kuwajenga na kuwaimarisha kiimani. Hivyo inaendesha program mbalimbali za kuwafundisha vijana, teenagers na watoto wadogo.

Huduma ya Teenagers

Huduma ya Teenagers ni kusanyiko la watoto wenye umri wa kuanzia miaka 13 mpaka 18, ambalo hukutana kila jumamosi saa 8 mchana mpaka saa 10 jioni. Walimu mbalimbali huwahudumia katika kuwajenga na kuwaiimarisha kiimani katika Kristo Yesu.  Msisitizo wa mafundisho haya ni katika kumjua Mungu, kujitambua na kuwa na maadili mema ili kuwajengea uwezo wa kukabiliana na maisha na kuwa na stadi za kushinda changamoto mbalimbali katika maisha. Pamoja na hayo tunawezesha kuendeleza na kuinua vipajina karama walizonazo.

Mafanikio ambayo yamepatikana

Vipindi hivi vimewajengea uwezo watoto wengi katika kujitambua, kujifunza zaidi juu ya Mungu, kuhusika katika kuujenga ufalme wa Mungu. Kutoa huduma kwa watoto wengine wa umri kama wao ambao wako katika mazingira hatarishi kama vile mahabusu ya watoto.

Pia hupata nafasi ya kuendeleza vipaji na karama mbalimbali walizo nazo.

Ratiba ya vipindi vyao

Kwa wiki mara moja- siku za Jumamosi saa 8 mchana

Nyakati za Likizo ndefu (Juni na Desemba)- siku za Jumatatu, Jumatano na Ijumaa saa 10 jioni

Pia huwa tuna semina za siku nzima kuanzia saa 3 mpaka saa 11 jioni.