HUDUMA YA VIJANA VYUONI

Mtume Onesmo Ndegi ambaye Mungu amemuita kufundisha Neno, ambayo ni Kweli ili kuweka watu huru, amekuwa akiyagusa makundi mengi hususani vijana.

Kupitia huduma  ya vijana walio vyuoni amekuwa akifundisha juu vijana kujitambua na kusimama katika nafasi zao kwa kuongeza ushirika wao na Mungu ili waweze kuujenga Ufalme wa Mungu kwa wepesi.

Vijana wa vyuoni ni kati ya kundi maalum ambalo Mtume Onesmo Ndegi amekuwa akilithamini kwa kutambua upekee wao hasa kwenye maendeleo ya taifa na ulimwengu kwa ujumla. Vijana wanaweza wakatumiwa vizuri na Kristo ama Shetani kutokana na nguvu walizo nazo. Hivyo ni jukumu la Kanisa kuwaendeleza kiroho ili watumie pia taaluma zao kwa manufaa ya Ufalme wa Kristo na wawe na maisha ya kuigwa kwa vizazi vijavyo.

Mtume Onesmo Ndegi amekuwa akifundisha vijana wa vyuo masomo mbalimbali kama vile HATMA (DESTINY), KUTAWALA NA KUMILIKI, MAOMBI, MAFANIKIO, IBADA HALISI (TRUE WORSHIP) n.k. Nia ni kutengeneza vijana ambao wana nguvu za Kiroho, Kiakili, Kiuchumi, Kiafya na Kimahusiano.

Wengi wa vijana ambao wamewahi kupata mafundisho ya jinsi hii na wameshamaliza masomo yao vyuoni, kwa sasa wana nafasi nyeti kwenye siasa/serikalini,  biashara, makampuni, makanisani na taasisi mbalimbali za uma na binafsi. Hii ni ndani na nje ya nchi.

Mpaka sasa huduma hii ya vyuoni inaendelea kwa kutambua Wito aliopewa na Mungu.