LIVING WATER CENTRE MINISTRY

marriage-2

MARRIAGE WORKSHOP 2

Viambatanishi vya Ndoa

 

Baada ya kuzijua kanuni tatu (3) muhimu  za ndoa, ni vyema sasa tukajifunza   viambatanishi vya ndoa. Mambo ambayo yanapaswa kufanyika wakati mnapotembea kwenye zile kanuni.

  1. KUTUMIKIANA

Wote mnazo haki sawa, nguvu sawa, na faida sawa. Chukua hatua za makusudi za kumfanya mwenzako ajisikie vizuri kuwa nawe.

Waza kumtumikia mwenzako. Mfanye afurahi. Usitake wewe kila saa ndio utumikiwe na kuwa bosi. Hakuna bosi kwenye ndoa! Yesu alisema anayetaka kuwa mkubwa na awe mtumishi wa wenzake. Kumbuka unapomtumika unatengeneza kibali chako kwa Bwana.

Ni muhimu pia kuwa na vipindi vya kufanya tathmini (evaluation) ya mahusiano yenu. Ambianeni ukweli na jali hoja ya mwenzako katika yale yanayomkera juu yako.

  1. KULINDANA

Usiruhusu maneno ya nje yatakayoharibu penzi lenu. Usikubali mtu amtukane mwenzi wako, amwaibishe hakikisha anakuwa salama. Kuwa na wajibu wa kumlinda hata akiwa hayupo. Hakikisha mwenzako yupo salama kiroho, kimwili, kiuchumi, kiafya na kiakili.

  1. KUTANGULIZANA

 

Mtangulize mwenzako katika mema yote. Mnunulie vitu vizuri, kumbuka akipendeza sifa ni kwako. Mjali mwenzako kuliko mtu mwingine yeyote. Mpe nafasi ya kwanza na yeye ajue hivyo.

  1. KUCHUKULIANA

 

Kila mtu huja na tabia zake, lazima kusaidiana, kuchukuliana, kuinuana tena kwa upole. Pale alipo dhaifu chukuliana naye, naye atachukuliana nawe katika madhaifu yako. Mpo ili kufaidiana.

  1. KUSIKILIZANA

Kumbuka mwanamke anapenda asikilizwe. Usidharau hoja zake, ukimsikiliza ataona unamjali. Jali kuponya moyo wake. Mnaposikilizana mtaepuka magomvi yasiyo na maana. Mnaposikilizana mtaweza kufanya mengi ya kimaendeleo. Peaneni nafasi za kuwa huru na mwenzako.

  1. KUHESHIMIANA

 

Kila mtu ampe mwenzake heshima.Tambua kuwa wewe ni mali yake na yeye ni mali yako. Unapomheshimu mwenzako na wanokuzunguka watamheshimu.

  1. KUHOFIANA

 

Ukimhofia mwenzako huwezi kumfanyia mambo mabaya wala kumkosesha.

CategoryMASOMO YA VIJANA
© 2016 Living Water Centre | Designed by Consuming Fire Technologies.
Top
Follow us: