LIVING WATER CENTRE MINISTRY

marriage-2

MARRIAGE WORKSHOP 1

Utangulizi

Mwanzo 2:18      Bwana Mungu akasemasi vyema mtu huyu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.

Ndoa sio mapenzi ya mwanadamu bali ya Mungu. Tumeikuta Ndoa, ni

mpango wa Mungu mwenyewe. Alianzisha kwa Makusudi yake sio sisi. Hii

ni Taasisi yake binafsi, ingawa unaweza kufanya kazi kwenye hiyo taasisi. Kimsingi Ndoa sio mali yako bali Yake. Mungu anakupa hiyo taasisi (ndoa) uitunze, uilee halafu umrudishie ikiwa na utukufu. Kumbuka mwenye mamlaka ya mwisho kwenye kampuni ni Yule mwenye kampuni. Kwa hiyo sisi ni waajiriwa wa Ndoa. Tumepewa ndamana na Mungu!

Mungu anakupa msaidizi wa kukufaa. Msaidizi wa kufanana nawe maana anakuja kukamilisha pale ulipo na mapungufu. Jinsi ulivyo ndivyo utampata mfanano wako. Kama wewe una usanii na ataletwa kwako msanii nanyi mtaishi kwenye jumba la sanaa. Mwenzi wako sio kitu cha kuchezea bali wa kumjali kama unavyojijali. Unapochezea ndoa unakuwa umechezea mpango mzima wa Mungu. Huishi kwenye ndoa kama upendavyo, bali kwa kanuni sahihi alizoweka Mwenyewe.

Ebrania 13:4       Ndoa na iheshimiwe na watu wote

Ndoa na iheshimiwe kuliko vyote

Ndoa ipewe heshima yote

Hakuna laana mbaya kuliko ya kuichezea ndoa. Lazima ndoa itunzwe kwa heshima, ipewe kicho (reverence). Ndoa ya wanaoelewana vizuri lazima maisha yao yawe na utoshelevu.

Mithali 18:22       Mke ni kibali

Unapopata mke umepata kibali, ukimtesa unapoteza kibali (favour). Jifunze kutunza na kuheshimu kibali. Uzuri wa kitu ni macho yako; ombea macho yako yaone mke wako ni mzuri kuliko wengine.

Malaki 2:16         Mungu anachukia kuachana

Siku zote kwenye ndoa watu hutaka kubadilishana,usijitahidi kumbadilisha tabia, utasababisha ligi. Njia nzuri ya kumbadilisha mwenzako ni kubadilika wewe kwanza. Mtafute Mungu katika Neno akubadilishe wewe, nawe utakuwa changamoto kwa mbadiliko ya mwenzako.

Kanuni muhimu kwenye Ndoa

 

Mwanzo 2:23-24 Adamu akasema sasa huyu ni  mifupa katika mifupa yangu na  nyama katika nyama yangu,basi ataitwa mwanamke. Kwa hiyo MWANAMUME atamwacha babaye na mamaye naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.

Zaburi 45:10       Sikia BINTI utazame utege sikio lako. Uwasahau watu wako na nyumba ya baba yako.

Mistari hii miwili inawazungumzia wote wawili wanandoa, na wale wanaowazunguka.

Kanuni ya I: KUONDOKA

 

Hii ni kanuni muhimu sana katika ndoa. Wote mnatakiwa muondoke! Na kama hujaondoka ni ngumu kuambatana. Hapa ni suala la kuacha utegemezi kwao (wazazi)na kuwa mtegemezi kwa mwenzi wako. Maamuzi yawe ni yenu sio yao na wanapotoa ushauri sio amri kwenu. Halafu wazazi hao wote wanakuwa wazazi wenu. Hakuna cha baba mkwe/mama mkwe bali wote ni wazazi.

Ukiondoka huwazagi kurudi ni mbele kwa mbele. Ni kama vile unapanda ngazi juu na ya chini inang’ooka.

Kesi nyingi za ndoa zinatokana na ubinafsi, unafiki na ubishi.

 

Kanuni ya II: KUAMBATANA

Mkishaondoka ndipo mnaweza kuambatana. Kuambatana ni kuwa na mambo yote kwa umoja. Usifanya mambo kwa siri. Mnakuwa shirika – umoja – uambatano. Mashamba, nyumba, mali, watoto, biashara, kazi, viwanya ni shirika. Hakuna unafiki, ndiyo yako ni ndiyo na siyo yako ni siyo. Kumbuka mtu pekee anayeweza kutunza familia yako ni mwenzi wako wakati ukiwa haupo, kwa hiyo mwaminishe na ulivyo navyo.

Kanuni ya III: KUWA MWILI MMOJA

Hii ni matokeo ya kanuni zote mbili zilizotangulia. Hamuwezi kuwa mwili mmoja kama hamjaondoka na kuambatana! Huwezi kuwa na mapenzi kamili kama hamjawa mwili mmoja. Kama unataka maneno kama Asante, Pole, Karibu, Nakupenda….. yawe na nguvu ni lazima kwanza muwe mwili mmoja.  Lazima ujisikie wewe ni sehemu yake na yeye ni sehemu yako.

Unakuwa na mzigo na mwenzako. Kinachomgusa yeye kimekugusa wewe. Hivyo utamlinda na kumjali asidhurike kwa lolote. Ni kama vile mtu akimgusa mke/mme wa wako amegusa jicho lako.

CategoryMASOMO YA VIJANA
© 2016 Living Water Centre | Designed by Consuming Fire Technologies.
Top
Follow us: