Huduma ya Watoto
Huduma ya watoto hapa Living Water centre Makuti Kawe, tunakutana kila jumapili katika ibada ya pili inayoanza saa tatu asubuhi. Watoto hujumuika pamoja na wazazi, na waumini wengine katika ibada ya pamoja ya kusifu na kuabudu, na baada ya hapo watoto huenda kwenye madarasa yao.
Huduma hii hujumuisha watoto wneye umri wa kuanzia miaka 3 mpaka 12. Watoto hukusanyika katika madarasa yao tofauti kulingana na umri wao kwa ajili ya kujifunza neno la Mungu. Huduma hii ina walimu 9.
Theme ya Huduma hii ni Kumjua Mungu, sawasawa na neno kutoka Yohana 17:3, na mission ni Kuenenda katika njia Itupasayo hata tutakapokuwa wazee.
MAFANIKIO
Tumefanikiwa kuwa na ibada za watoto kila jumapili na Mungu ametuwezesha kuweza kufundisha Neno lake kwa neema ya ajabu.