LIVING WATER CENTRE MINISTRY

praisejesus

JINSI YA KUIFANYA KESHO (HATMA) ILIYOFANIKIWA

(Mwl Lilian Ndegi, KAMBI YA VIJANA 16 Jan 16)

Ujana ndio umri ulio mfupi kuliko rika lingine; sio zaidi ya miaka 15. Kijana jitambue kuwa upo kwenye safari,hivyo jifunze kutazama mbele. Jicho lako litazame kesho yako tokea hapo ulipo.

Ikiwa hatmahutengenezwa, basi usifanye kwa udhaifu. Kile unachokitaka baadaye, haakikisha unakifanya sahivi.

Moyo wa kumpenda Mungu, ndio humfanya aachilie kibali na ukuu kwako.

Mithali 23:7 Ujionavyo nafsini yaani ujionavyo ndani yako.

Jinsi unavyojiona kutokea ndani yako ndivyo ulivyo. Macho ya ndani yanaweza kuona kesho yangu. Hatma yangu ni vile nijionavyo. Hatma yangu haitoki kwa wanadamu kama vile wazazi. Hakikisha unaona na kujiona jinsi Mungu aonavyo na akuonavyo. Maisha yetu yalikwisha kupangiliwa tayari na Mungu, hivyo ishi kwa kufuata hicho. Usiruhusu kikwazo chochote ulichonacho sahivi kukuzuia kuifikia hatma yako. Hatma yako kijana imefungwa katika vile uonavyo kwa macho ya ndani. Hakuna kubahatisha katika maisha.

Ili kupata Hatma iliyofanikiwa unahitaji:-

  1. Nguvu ya kufikiri tofauti

Fikra au Thinking is to fix your mind on or take account of things. Kuweka maanani na kutilia mkazo (katika ufahamu) kitu fulani.

Kila kitu uonacho ni nguvu ya fikra ama ni matokeo ya kufikiri. Sisi kama wakristo yatupasa kuwa wabunifu. Ukishafikiri hakikisha unachukua hatua za utendaji ili uone matunda. Mtaji wako ni fikra zako. Fikiri kutengenezea watu ajira, maisha na mafanikio.

Mwanzo 11:6 Na haya ndiyo wanayoanza kufikiri. Mtu anayefikiri hawezi kuzuiliwa wala kushindwa.

Luka 14:28 Unajenga kwa kile tayari ulichofikiri.

Usiwe mvivu wa kufikiri na weka umakini katika kufikiri. Jifunze kufikiri na weka umakini katika kufikiri. Jifunze kufikiri kwaupya,hasa pale makosa yanapotokea.

Mithali 24:27   kuna maandalizi ya fikra kwanza ndipo ujenge

Fikiri tofauti mara zote. Mtu anayefikiri hakurupuki. Usitafute njia za mkato. Mwenye fikra hujivumbua uwezo alionao na pia kumpa usahihi wa kufanya maamuzi. Unahitaji kufikiri sana kabla ya kufanya maamuzi. Kufikiri hukupa kuona mwanga mahali penye giza.

Matunda ya kufikiri katika usahihi

  1. Mtu mwenye kufikiri huwa na mtazamo sahihi
  2. Mtu mwenye kufikiri huambatana na mtu sahihi
  1. Mtu anayekwenda kwenye hatma ya kufanikiwa,ana uwezo wa kufanya kazi. Usipofanya kazi, unahesabika kama mdhambi.

Huu ni mwaka wa kazi.

Mhubiri 10:18  Mahali pa uvivu, pana uharibifu, patavuja.

Mwili wangu unapaswa kufanya kazi. Sio kulalalala. Fedha inapaswa kunifuata mahali pa kazi sio kitandani. Lazima nionyeshe moyo wa kufanya kazi. Mungu hufanya kazi na mtu anayefanya kazi.

Mithali 10:4 Ili kutegua kitendawili cha umaskini,ni lazima kufanya kazi

Kukosa fedha ni kitu kibaya sana.

Mithali 10:16 mtu mwenye haki unapaswa kuwa na kazi, maana huelekea mafanikio. Penda hiyo kazi na moyo wako uwe hapo, ndipo utabarikiwa na hutakuwa na manung’uniko tena.

Mithali 20:13 tatizo sio kulala bali kupenda usingizi

Ukipenda usingizi utachukia kazi. Jifunze kulala tu kwa ajili ya afay ya mwili.

Mithali 13:4 Kutamani tu hakukupi kitu bali kazi ndiyo hukupa jibu.

Ufalme wa Mungu hapa duniani unahitaji  fedha, na unapoikosa ni kuuathiri na kuonyesha kwamba bado wewe  hujafanikiwa. Tafuta kwa ajili ya Bwana na yako.

CategoryMASOMO YA VIJANA
© 2016 Living Water Centre | Designed by Consuming Fire Technologies.
Top
Follow us: