LIVING WATER CENTRE MINISTRY

160113_friendship

JINSI YA KUENDESHA MAISHA YA UCHUMBA

(Mwl Diana Mndeme, Kambi ya Vijana 16 Jan 16)

Warumi 12:2  Hata katika maisha ya uchumba, sipaswi kuifuatisha namna ya dunia hii, bali ugeuzwe kwa kufanywa upya nia yako.

Ipo namna ya dunia hii katika masuala ya kuendesha uchumba, na pia ipo namna ya Kimungu vile vile. Sisi watoto wa Mungu, yatupasa tufanye kwa maelekezo ya Baba yetu ili tuwe salama sasa na baadaye.

Hapa lazima kugeuzwa kwanza nia yako ndipo uweze kuyafanya mapenzi yake Mungu.Kitu chochote kisichotokana na Neno la Mungu hakiwezi kuwa kanuni; hata kama watu wanakifanya.

Uchumba ni kipindi muhimu sana katika kujenga msingi wa ndoa. Unapoingia katika ndoa, utavuna ulichopanda katika uchumba. Jiulize maswali yafuatayo:-

  1. Je, uchumba wako upo tofauti na wa mataifa?
  2. Je, Mungu anajivunia huo uchumba kwenye maisha yenu ya sirini na hadharani?

Uchumba ni kipindi pia cha kuwapa fursa ya kufahamiana.  Kipindi hiki unatengenezwa kuwa bora kwa ajili ya mwenzako.Kumbuka unapoingia katika ndoa, unakwenda kuitumikia hiyo taasisi ya ndoa. Achana na ubinafsi. Tafuta kuwa bora kwa ajili ya utumishi huo.

Kipindi hiki ni cha kujenga misuli ya kiroho  (spiritual muscles).

Duniani mfumo wa kuendesha uchumba hauna mipaka kabisa, hautofautiani kama katika ndoa. Watu wanalala pamoja, wanamiliki pamoja, wanapikiana, n.k. Hii ni kufanya mambo kwa ufahamu usio sahihi.

Efeso 5:31 Kwenye ndoa ndipo mnapopaswa kuwa vitu vyote shirika (huku kunaitwa kuambatana)

Dunia huendesha uchumba kwa tama.Katika ufalme wa Mungu inawezekana kuishi bila zinaa. Ni suala la mtazamo na kukiri sahihi, na kumwamini Mungu atendaye kazi tokea ndani yako.

I Korintho 6:18 Mungu anapozungumza hututofautisha na ulimwengu.

Jiulize, Yakobo aliwezaje kuishi nyumba moja na mchumba wake? Tena pasipo kuanguka katika dhambi! Tena kipindi kabla ya Roho Mtakatifu kuja kuishi ndani yao kama ilivyo kwetu leo! Kama Yakobo aliweza kuendesha uchumba kwa utakatifu, hata mimi nitaweza kwa kuwa ni bora zaidi.

Wimbo ulio bora 2:7 usilazimishe wala kuchochea tamaa za mwili.

Kumbuka hatuingii katika ndoa kwa ajili yetu wenyewe, bali sana kwa ajili ya utukufu na kusudi la Mungu. Usiwe na hofu yoyote; umri, sura, mapishi n.k

Mwanzo 2:20-25 Lala usingizi mzito ili Bwana akuandalie akufaaye.

Hili suala la ndoa sio la kulazimisha sana, usije ukahatarisha maisha yako.

Mwanzo 24:7,12 Suala la kutafuta mwenzi ni la Mungu lote.

Hata ukimchunguza tabia bado hutammaliza na watu huzidi kubadilika; hivyo unamwitaji Mungu katika hili.

Mwana wa Mungu anapoombea kuhusu mwenzi ni tofauti na mataifa, kwani sisi tunamwitaji yule atakayekamilisha na tutakayekamilisha Makusudi pamoja.

Mathayo 6:33

Madhara ya kuendesha uchumba isivyofaa

  1. Mnakuwa mmemfungulia adui mlango wa yeye kwenda nanyi hadi kwenye ndoa.
  2. Hatia inazalishwa
  3. Msukosuko wa kiroho. Kuacha wokovu kabisa.
  4. Maisha magumu katika ndoa

#Kitu pekee cha kusaidia kuendesha Uchumba ni: LIFAHAMU KUSUDI LA MUNGU,  MHUSISHE MUNGU, FANYA TATHMINI NA USIFUATISHE NAMNA YA ULIMWEMNGU.

 
CategoryMASOMO YA VIJANA
© 2016 Living Water Centre | Designed by Consuming Fire Technologies.
Top
Follow us: