LIVING WATER CENTRE MINISTRY

Jesus-washing-feet

FAIDA YA KUMTUMIKIA MUNGU KATIKA UJANA

(Pastor Shenyagwa, KAMBI YA VIJANA 16 Jan 16)

Yeremia 1:4-6   Yeremia aliitwa kumtumikia Mungu tangu akiwa  mdogo

Mungu mahali pengi aliita watumishi wengi tangu wakiwa vijana.

I Samweli 16:13      I Samweli 3:1          Isaya 6:5       Waamuzi 6:1

Vijana wengi hukataa wanapoitwa hujiona wadhaifu.Changamoto walizo nazo wanapoitwa ni kujiona wadogo, dhaifu, wanyonge, hawataweza, ni duni n.k

Kwa nini Mungu aite watu tokea ujanani?

  1. Hutaka kumtengeneza huyu kijana kabla hajaanza kumtumia Yeremia 1:9
  2. Hutaka kumtakasa kabla ya kumtumia Isaya 6:5-6
  3. Hutaka akufundishe vya kutosha Kutoka 3

Mungu kabla ya kukutumia atakufundisha na ataendelea kukufundisha

Chunguza safari yako

  1. Tambua uwepo wa “Eli” wako. Baba wa kiroho hukuwezesha kuijua sauti ya Mungu ili uweze kumtumikia.

Hakuna mafanikio katika utumishi wako kama hukubali kukaa chini ya baba wa kiroho. Kumbuka maua hata yawe mazuri kiasi gani, yakitolewa kwenye shina hayachukui muda ila hunyauka na kufa. Kwa sababu ustawi wa ua hutegemea kukaa kwake katika shina.Unamwitaji sana baba wa kiroho.

  1. Jiunganishe naye kwa kumsikiliza na kumtii.

Fanya kazi kwenye ufalme. Kipindi cha ‘weekends’, likizo huwa unakitumiaje? Kipindi hiki cha ujana usichague kazi katika ufalme, fanya yoyote wakuagizayo. Ni kipindi cha ukuruta.Ila onyesha ufasaha na bidii nyingi. Jenga moyo wa kazi.

  1. Toa moyo wako kwa njia ya matoleo

Hakikisha unafanya kazi ya kuingiza kipato ili uwe na kitu cha kutoa kwenye ufalme. Ufalme unahitaji pesa nyingi, na pesa hiyo wewe ndiye wa kuileta. Kumbuka fedha yako ilipo ndipo na moyo wako unapokuwepo. Hivyo, unapowekeza fedha yako katika ufalme, moyo wako ndipo unapodumu hapo, na Mungu ndipo anapokutana nawe. Wanohitajika wa kwanza kuendesha ufalme, ni vijana. Kijana uwe mwainifu katika fungu la kumi,na sadaka nyinginezo.

Faida za kumtumikia Mungu ujanani

  1. Mungu ataushibisha uzee wako mema Zaburi 103:1-5

Zaburi 68:19 Mtumikie Mungu siku kwa siku. Yoshua 14:11 Mzee Kalebu alikumbukwa na kupewa urithi kwa yale aliyoyaishi ujanani mwake

  1. Unakuwa huku ukitakaswa

Zaburi 119:9 Ongeza shauku ya Neno

  1. Unakuwa katika Neema ya kumtumikia Mungu
  1. Uwepo wake hukufanya uwe na furaha na utakatifu

I Korintho 1:9

CategoryMASOMO YA VIJANA
© 2016 Living Water Centre | Designed by Consuming Fire Technologies.
Top
Follow us: