12804861_1046750838705044_5185641845071322879_nHii ni huduma ya Kikristo inayoongozwa na Mtumishi wa Mungu, Mtume Onesmo Ndegi, pamoja na Pastor Lilian Ndegi wakishirikiana na Watenda Kazi wengine kikiwemo kikundi kazi cha Bwana cha Kusifu na kumwabudu Mungu, kiitwacho Living Waters.

Katika Tovuti hii tutakuletea Habari, Masomo, Matukio na Ratiba zetu mbalimbali zinazoendelea katika Huduma hii ya Living Water Centre – Makuti Kawe.

Waweza kuabudu pamoja nasi Living Water Centre – Makuti Kawe au katika Makanisa yetu yaliopo katika Mikoa Mbali Mbali Tanzania, na mengine mengi jijini Dar es Salaam na hakika utamjua Bwana zaidi na kiwango chako cha ushirika na Yeye kitakuwa juu zaidi.

Karibu na Mungu akubariki sana

MAONO (VISION)

Kusimamisha Ufalme wa Mungu ndani na nje ya Tanzania.

MKAKATI (MISSION)

Kutengeneza Kanisa ambalo Mungu alilokusudia kwa kuwafikia wengi kupitia Fundisho la Kweli linalowaleta watu kwa Mungu.

LENGO LA MISSION

  • Kuwa na badiliko la maana la kiroho la Kanisa kwa kuwafanya wanafunzi na fundisho la Kweli.
  • Kutengeneza timu ya watendakazi ambao wamejitoa kutoa huduma na kufundisha wengine kuwa viongozi (watumishi).
  • Kuwabariki wengine kwa kuwapa vitu/huduma wale wenye uhitaji kama mavazi, elimu, makazi, chakula na afya.
  • Kuufikia ulimwengu na Habari Njema kwa kuwa na ushirika na Mungu.